About Kisukari
Kisukari (Jina la kitaalamu: DIABETES MELLITUS) ni ugonjwa unaoonyesha viwango vikubwa vya glukosi katika damu. Sababu yake ni uhaba wa homoni ya Insulini mwilini au upungufu wa uwezo wa mwili wa kukubali Insulini.
Watu wachache huzaliwa na uhaba wa insulini. Watu walio wengi wana udhaifu fulani unaokuwa hatari kutokana na aina za vyakula na maisha ya kila siku. Kutumia sukari nyingi pamoja na mafuta mengi katika chakula na vinywaji, kukosa mazoezi ya mwili (kwa watu wenye kazi ofisini), kunywa pombe nyingi na uvutaji sigara huongeza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari baada ya miaka ya ujana.
Pia ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa matatizo ya muda mrefu na mfupi mwilini kutokana na upungufu au kutoweza kutumika vizuri kwa kichocheo kinachoitwa Insulini. Insulini hutengenezwa na chembechembe zilizopo ndani ya kiungo cha kongosho. Miili yetu inahitaji isulini ili kuweza kutumia sukari tuliyonayo mwilini. Sukari inatokana na chakula ambacho tunakula kila siku na hutumika kwa kutupa nguvu mwilini. Kwa kawaida sukari Ikizidi, ya ziada inahifadhiwa katika ini kama mafuta. Mafuta haya hubadilishwa kuwa sukari na kutumika wakati tukiwa na njaa kwa muda mrefu. Endapo kuna matatizo ya kutengeneza au kutumika kwa insulin, sukari mwilini huongezeka haraka na inamaanisha ugonjwa wa kisukari apo na dalili kuanza kuonekana.
Nukuu:
Imeelezwa kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wanaugua ugonjwa wa kisukari hali ambayo huchangiwa na unywaji wa pombe, huvutaji wa sigara, ulaji wa vyakula usiofaa na kutokufanya mazoezi ya mwili. Hayo yalisemwa na Dk. Omary Ubuguyu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari kuhusu ugonjwa huo jijini Dares Salaam. Aliongeza kuwa asilimia ya idadi ya watu 80 hadi 90 wanaugua ugonjwa huo duniani. “ Unywaji wa pombe kuanzia chupa tano kwa wanaume na chupa 4 kwa wanawake huchangia kusababisha ugonjwa huu,” alisema Dk. Ubuguyu.
by N####:
Good looking and arangement. From this we learn much.